GET /api/v0.1/hansard/entries/781247/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 781247,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/781247/?format=api",
"text_counter": 71,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana, Bwana Spika. Ningependa pia kuchangia Petition hii. Bw. Spika, swala la Standard Gauge Railway (SGR) ni nzuri katika nchi yetu ya Kenya, lakini limeweza kubadilisha maisha ya watu katika nyanja tofauti. Imebidi watu wahame mashamba na ploti zao ili SGR iweze kupata nafasi ya kupita. Tunaona malipo ya ridhaa yaongezwe kwa sababu yamekuwa duni na yanatofautiana kila mahali. Kwa mfano, upande wa Changamwe, watu wanalipwa kiasi tofauti na upande wa Mariakani au Mikindani. Serikali inafaa kuunda mikakati mwafaka ili wananchi wanaoishi katika sehemu ambazo SGR inapitia wajue jinsi watakavyolipwa pesa zao. Haifai wengine kulipwa laki mbili, wengine laki moja na wengine nusu laki. Hiyo si haki. Watu lazima walipwe kisawa. Sio kulipwa kulingana na pahali wanapoishi. Bw. Spika, reli ya SGR isitumike kama kielelezo cha kuua Bandari ya Mombasa. Hivi sasa, kunayo maoni ya kwamba, Bandari ya Mombasa itakufa."
}