GET /api/v0.1/hansard/entries/782172/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 782172,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/782172/?format=api",
    "text_counter": 39,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Ahsante Bw. Spika. Ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza Sen. Orengo kwa kuchaguliwa kama kiongozi wawalio wachache katika Bunge hili la Seneti. Kwa hakika, Sen. Orengo alisimama kidete kwa upande wa upinzani. Rekodi zake zimejiandika na kwa hakika, wakati kulikuwa na vuta nikuvute katika kinyang’anyiro cha uchaguzi, Sen. Orengo aligonga vichwa vya habari na kuweza kupeleka sehemu ile yake mbele. Sen. Orengo anafaa katika cheo ambacho amechaguliwa na kwa wakati huu, tunamkaribisha kuongozi wa wale walio wachache katika Bunge hii la Seneti. Ningependa pia kueleza masikitiko yangu kwa rafiki yangu, Seneta Wetangula, ambaye aliongoza Maseneta walio wachache katika ugatuzi wa kwanza katika Bunge hilo kwa miaka mitano mpaka kufikia ugatuzi wa pili na siku ya leo. Kwa hakika, Seneta Wetangula aliendesha kazi na Ofisi hiyo kwa ujasiri kubwa sana na aliweza kuusukuma upande huu wa Serikali kwa nguvu zake zote. Kwa wakati huu, singependa kuchochea upande wa upinzani; lakini kilio huanza kwa wenyewe. Kilio kikianza kwa wenyewe, wanaofariji wakiongezeka, wataanza kilio hicho na pia sisi hatuna budi kulia na wao. Mumetoa uamuzi na sisi pia tunasema tuko pamoja na nyinyi, kwa sababu wengi wape na wale wachache pia wako na njia yao ya kupita. Kwa sababu hiyo, Seneta Wetangula, bado utabaki hapa; ukisukumwa sana, tunahitaji zile debate na hoja zako nzuri nzuri unazotoa. Usikae kwenye baridi sana; unaweza vuka upande hii ukaja---"
}