GET /api/v0.1/hansard/entries/783073/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 783073,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783073/?format=api",
"text_counter": 535,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Jambo la kwanza, nasimama kupinga ripoti hii. Tunaelewa kwamba katika maisha ya binadamu, urefu, ufupi na miaka ya kuishi katika ulimwengu ni ya Mwenyezi Mungu. Katika maisha, huwezi hata kidogo kumbaguwa mtu kwa sababu yeye ni mfupi au mrefu. Hayo ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Tukiangalia ripoti, tunaona kwamba Sen. Melly ni kijana mdogo sana. Lakini, kuwa kijana haimaanishi hana akili na ndio maana aliitwa katika mahojiano na baada ya hayo, mwenyekiti, naibu wake na kamati nzima tunayoifahamu na tuliipa jukumu hilo walimualika na baadaye wakahakikisha ameibuka mshindi. Hivi leo ni jambo la kusikitisha kabisa kuona katika Seneti, mmoja wetu ambaye amefuzu anatengwa kwa sababu ya umri wake. Watu wa Kaunti ya Uasin Gishu mwaka wa 2013, katika maeneo ya Bunge saba yaliyoko katika kaunti hiyo, walimchagua kijana mdogo kuja hapa na akafanya kazi miaka mitano bila kushindwa. Jambo kuu ni kwamba tusimtoe Sen. Melly kwa sababu yeye ni mfupi, miaka yake haijatosha au pengine ni mrefu. Kama mtu ameibuka wa kwanza katika mahojiano, ni haki hata mbele ya Mwenyezi Mungu apewe kazi hiyo. Haijalishi Sen. Melly ni mdogo ama mkubwa; haki yake apewe."
}