GET /api/v0.1/hansard/entries/783117/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 783117,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783117/?format=api",
"text_counter": 579,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwa Kiswahili tunasema ‘uzoefu wa awali.’ Kwa hivyo, uzoefu wake wa awali ulitiliwa maanani kwamba alikuwa amefanya kazi kama msimamizai wa maswala ya wanafunzi katika chuo kikuu na pia amekuwa Seneta kwa wa miaka mitano. Ijapokuwa ripoti inasema kuwa ana uzoefu wa awali wa miaka kumi kwa mambo ya fedha ilivyotakikana na Section 5 (2) (b), aliweza kuwashinda wenzake kwa alama tatu. Kwa hivyo, inaonekana kwamba huyu ni mwerevu. Tunaweza kumuita kwa kiingereza genius kulingana na mahojiano yaliyofanyika. Bwana, Spika wa muda, naunga mkono kwamba tubadilishe majina ya Sen. Isack Kipkemboi Melly na Bi. Margaret Sawe wakubaliwe kama washindani kwa nafasi hii ya mwakilishi wa kaunti katika Salaries and Remuneration Commission (SRC)."
}