GET /api/v0.1/hansard/entries/783228/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 783228,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783228/?format=api",
    "text_counter": 60,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13398,
        "legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
        "slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, shukrani sana. Naomba nianze kwa kusema kuwa naunga mkono Hoja hii kuhusu maafisa wa polisi. Sharti masuala yao yaungwe mkono. Nitaanza kwa kusema kuwa dunia nzima imewekeza vilivyo katika usalama wa taifa lakini hapa nchini Kenya, sisi tumewekeza katika uhalifu wa kujitakia kwa sababu hatufuatilii utaratibu na kanuni zinazohitajika kuhakikisha kwamba usalama wa taifa unapatikana. Polisi ni mwananchi. Pia ni raia wa kawaida kama Mkenya mwingine. Kwa hivyo, polisi wanahitaji kuangaliwa vilivyo ili waweze kutulinda sisi Wakenya."
}