GET /api/v0.1/hansard/entries/783229/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 783229,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783229/?format=api",
    "text_counter": 61,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13398,
        "legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
        "slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
    },
    "content": "Pia nitazungumzia masuala kama vile bima yao, vifaa wanavyotumia, nyumba wanamoishi, mishahara yao pamoja na marupurupu wanayopata. Maafisa wa polisi wanalipwa vibaya mno. Hata askari gongo analipwa zaidi ya afisa wa polisi. Ndio maana unaona nchi hii haisongi mbele kwa sababu hatuekezi katika usalama wa taifa. Ningelipenda kutoa mifano ambayo ni ya muhimu zaidi, hususa katika vituo vya polisi au kambi za polisi. Vile maafisa wa polisi wanavyoishi ni jambo la kuchukiza mno. Vyumba wanavyotumia ni vyumba ambavyo aliyeoa na asiyeoa wanaishi pamoja. Huyu ambaye ameoa akitumwa safari ya mbali kwenda kuhudumia taifa, kuna mtu anajenga nyumba yake. Ataregea kwa hasira na kufanya mambo ya ajabu ajabu kama kuua au kufanya mambo mengine kisha tutaanza kupiga kelele na kusema kuwa maafisa wa polisi hawafanyi kazi inavyotakikana. Sisi Wabunge twapaswa kuweka mfano bora katika Bunge hili na kuhakikisha kwamba Hoja hii imepita na maafisa wa polisi wameanza kulipwa kama maafisa wengine. Tuweke mfano bora kwa maafisa wa polisi wanaotulinda ambao wanakaa hapa nje na ambao kunyeshewa au kuwe na jua kali, wanasimama tu hapa nje wala hawana mahala hata pa kujizuia. Tuanze kwa kuweka mfano bora na watu kama hawa. Kuna maafisa chapakazi walioumia kwa ajili ya taifa hili. Namkumbuka afisa wa polisi Erastus Kirui Chemorei aliyepigwa risasi 21 kule Kitale na ambaye hadi sasa amezikwa katika kaburi kama mhalifu ilhali yeye si mhalifu. Ni mtu aliyekuwa akilinda maslahi ya Wakenya. Namkumbuka afisa wa polisi aliyemuangamiza jambazi sugu zaidi aliyeitwa Rasta. Yuko Eldoret hadi sasa hivi. Ana risasi mwilini mwake. Hadi wa leo, hajapewa heshima wala matibabu ya kutolewa risasi hiyo kwa kazi aliyowafanyia Wakenya. Ni nani atakayezungumza kuhusu maafisa wa polisi 40 waliouawa kule Baragoi? Nilikuwa pale kama mwanahabari kuangazia masahibu ya maafisa wa polisi. Waliuawa kinyama. Hakuna mtu yeyote anayewazungumzia kuhusu maafisa wengine 29 waliouawa kule Kasarani, Turkana. Hawa ni watu wa kawaida. Hawa ni Wakenya na ni binadamu. Watu hawa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}