GET /api/v0.1/hansard/entries/783230/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 783230,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783230/?format=api",
"text_counter": 62,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13398,
"legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
"slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
},
"content": "wana familia. Hatutakaa tukiimba kila siku kuanzia Januari hadi Disemba tukizungumzia masuala ya nyongeza ya mshahara ya maafisa wa polisi. Haifai. Haikubaliki. Hawa ni binadamu ambao wana uzito wa kutulinda sisi na taifa nzima. Leo, afisa wa polisi analipwa kati ya Ksh15,000 na Ksh21,000. Ukiweka zote kwa pamoja - Ksh15, 000 au Ksh21, 000 - atapeleka wapi? Hi ni kama chakula chako cha mchana. Ana watoto na bibi. Hawajui watoto wao wataenda shule gani. Katika kambi za jeshi, angalau wamejaribu kuekeza katika elimu na kujenga shule zao. Kambi za jeshi zina shule. Polisi hawana. Watoto wa polisi wataenda wapi? Leo, bibi wa polisi akipachikwa mimba atajisaidia wapi? Hana bima. Ndio maana polisi anarudi katika ile kauli mbiu yake ya bima yake: “toa kitu kidogo”. Kwa sababu sisi tumeshindwa kutunga sheria ya kuwafikia hao watu. Wakati ambapo polisi ni mtu wa maana katika taifa hili, ni wakati ambapo kuna uvamizi Kenya. Katika shambulio la kigaidi kule Westgate, maafisa wa polisi walijizatiti wakahakikisha ya kwamba wamelinda maslahi ya Wakenya. Maafisa wale wote waliopigana pale katika jumba la Westgate bado wana makovu ya upweke, bado hawajalipwa na bado wanatembea na machungu kwa sababu hawawezi fikia hospitali. Afisa ambaye amepigwa risasi akipambana na mhalifu anaambiwa ajipeleke katika Hospitali ya Kenyatta. Hapewi heshima ya afisa wa polisi. Ni kwa sababu sisi hatutaki kutunga hizo sheria. Lau kama tungetunga sheria za kuleta mambo ya anasa duniani, tungelikuwa wa kwanza kuzipitisha haraka haraka. Lakini sheria ambazo zinahusu maisha ya watu hawa hatufanyi. Naomba tuweke mfano na hawa wanaotulinda. Naomba tuwajengee mahala ambapo watakaa kwenye kivuli ili mvua ikinyesha wanaweza kujistiri mahali wakitusubiri. Ni lazima tutoe mfano kwa watu hawa. Leo wafisadi wakubwa na wabakaji wa demokrasia ni sisi Wabunge, Mawaziri na viongozi wengine wakubwa wakubwa. Lakini leo, afisa wa polisi wa barabarani akishikwa kama amechukua Ksh200, inakuwa ni habari ya dunia. Tunaacha wale walioiba mamilioni ya pesa; waliobeba na gunia, wakabeba; waliobeba na mabegi, wakabeba; lakini afisa wa polisi anayeiba Ksh200 tu, inakuwa ni taarifa za dunia. Kuna sababu ya yeye kuchukua Ksh200. Kwa sababu wewe huwezi kuishi Kenya sasa na mshahara wa Ksh15,000 au Ksh21,000, una bibi na watoto na unataka wawe na maisha kama ya Wakenya wengine. Hili ni jambo ambalo tunafaa tulifikirie zaidi na tulipitishe kwa haraka bila wasiwasi wowote. Kuna kitu wanaita Harambee SACCO. Hii si SACCO ya maafisa wa polisi; ni SACCO ya matapeli. Maafisa wa polisi wanaekeza pale lakini hizo pesa zinakuwa ni za kushurutishwa na zinatumiwa na baadhi ya maafisa wakuu wa polisi wanaowanyanyasa maafisa wadogo wa polisi. Hawapati marupurupu ya kazi ngumu au hardship allowance ambayo wanapaswa kulipwa wakienda katika sehemu mbalimbali hatari kwa usalama. Afisa atapelekwa sehemu kama Mandera au Kainuk kule Turkana na zile pesa ambazo anafaa alipwe kwa siku hawezi kupewa kwa sababu zinaingia katika mfuko wa afisa mmoja ambaye anajiona yeye ndiye simba kati ya maafisa wengine. Naomba kupendekeza Hoja hii ipitishwe. Angalau, nina furaha kama Mkenya kwa sababu tumeweza kufika kiwango cha dunia cha afisa mmoja kwa Wakenya 400, ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambayo hatukuweza kufika kiwango hiki. Kwa hivi sasa, Kenya nzima ina maafisa 80, 000 ambao wanalinda Wakenya milioni 45. Kuwapa motisha ni kuhakikisha kwamba wanapata mshahara wa kutosha ili waweze kujimudu wao na familia zao ili waweze kutuhudumia sisi Wakenya. Mvua inanyesha kila siku, jua ni kali lakini ukipita katika mabarabara yetu, utapata maafisa wamesimama kwa mvua. Hata Kitengo cha Usalama hakiwezi kuwapatia hawa watu mwavuli au majaketi ya kuzuia baridi. Ni laana na jambo la kuaibisha na kusikitisha. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}