GET /api/v0.1/hansard/entries/783231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 783231,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783231/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13398,
"legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
"slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
},
"content": "Nasimama na kusema kuwa wakati umefika wa Bunge hili la 12 kuhakikisha kwamba Hoja hii imepita na maafisa wa polisi wamehudumiwa. Tume ya Kavuludi isiwe tu ya vyombo vya habari. Iwe ni tume ya kuhakikisha ya kwamba hawa watu wamesikizwa na kulipwa ipasavyo. Hawa watu na ni binadamu. Hawana bima. Lazima washughulikiwe ipasavyo ili tuweze kuunda taifa nzuri ya usalama na kuekeza katika usalama kama nchi zingine. Dunia inaekeza katika usalama ilhali sisi tunaekeza katika ujinga. Leo, tunavamiwa kiholelaholela. Leo, utampa polisi bunduki aina ya bastola ambayo ina risasi 12 na jambazi ana bunduki aina ya AK47 na amejihami na risasi za kisasa. Leo, unawatuma maafisa kama hao wapambane na wahalifu wakubwa. Wapeeni silaha, vifaa, mshahara, na mambo yatakuwa mazuri."
}