GET /api/v0.1/hansard/entries/783297/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 783297,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783297/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. King’ara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13468,
"legal_name": "Simon Nganga Kingara",
"slug": "simon-nganga-kingara-2"
},
"content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa mwanya kuchangia Hoja hii muhimu kuhusu kazi ya askari wetu hapa nchini. Sitasema mengi kwa vile wenzangu Waheshimiwa wamegusia. Nitagusia mawili matatu ili niwape wengine nafasi kuchangia pia. La muhimu ni kwamba ukiangalia idadi ya wale askari wanatufanyia kazi, haswa viongozi, wanakaa maeneo duni sana. Isitoshe, idadi ya askari wanaotufanyia kazi ni haba mno. Nimesema hapa mara kwa mara kwamba tuko zaidi ya watu 500,000 katika eneo langu la Ruiru. Idadi ya askari wanaotuchunga Ruiru ni 153. Ukiangalia hicho kitengo, utapata askari mmoja anachunga watu zaidi ya 3,000. Hata kama anataka kufanya kazi, itakuwa vigumu kufanya kazi vilivyo. Ndiposa tunawalaumu. Lawama kwa askari iko juu kuliko kazi yao. Pili, kwa sababu ya uhaba wa hawa askari, itabidi watumikie wananchi, utakuta askari anafanya kazi usiku na mchana. Wakati anafanya hii kazi, hatembei mikono mtupu; huwa amebeba bunduki ya kilo kumi au zaidi. Naskia wengine wanasema amesomeshwa kufanya hivyo. Lakini, mwili ni wa binadamu. Tuheshimu hiyo. Hata kabla hatujaongea juu ya makazi ya askari wetu, wacha kwanza tuangalie wanafanya kazi wakitumia kiwango kipi cha utu. Hilo ni jambo litaleta usawa wa hawa askari kutufanyia kazi na sisi kufanyiwa kazi na wao. Labda hilo ndilo jambo linagusia hawa askari kutumia bunduki kiholela. Nafikiria imetokana na hasira. Hawa ni binadamu."
}