GET /api/v0.1/hansard/entries/783306/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 783306,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783306/?format=api",
"text_counter": 138,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. King’ara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13468,
"legal_name": "Simon Nganga Kingara",
"slug": "simon-nganga-kingara-2"
},
"content": "Nilikuwa nasema hivi, nitarudia ili asikie vizuri kwa sababu hili ni jambo muhimu. Linahusu binadamu kama mimi. Nimesema askari, hata kama wameenda chuoni, kufunzwa na kufanya utafiti kuhusu afya yao na ni nini wanaweza kubeba, wanastahili kula vizuri. Kama eneo la kufanyia kazi halitoi nafasi ya kukaa na kuwa na afya nzuri, atawezaje kufanya kazi? Labda siku fafanua vizuri. Hilo ndilo fafanuzi langu. Naomba tusichukulie hili jambo kwa mzaha. Hapa nje ya Jumba hili, mtu anayengojea kunisaidia kufika kwangu, kwa nyumba, kwa kuwa nitatoka hapa saa moja usiku, ni yule askari atanizindikisha. Kama riziki yake ni mbaya, roho ya kunitunza iko wapi? Kwa hivyo, hata kama si kuongeza mshahara, ni vizuri tuangalie hawa askari wetu watakaa vipi ili wapende kazi zao na nchi yao. Hata kama sitatoa matamshi yale yataleta uzito kuonyesha sababu ya kuangalia mjadala huu na kutafuta njia mwafaka ya kukaa na askari wetu. Tafadhalini, watu wengine wachangie tupatie askari wetu nafasi ya kukaa vizuri na kufanya kazi vizuri. Nilifurahia wakati kuliletwa mabadiliko kidogo na Mheshimiwa mwenzangu pale aligusia kwa kusema kuwa hata kama kuna maeneo yameumia zaidi, shida iko Kenya yote kwa jumla. Hivyo, ni sisi na wale wako hapa, kabla kuisha kwa mjadala huu, waendelee kuchangia na kuona wameleta yale mambo muhimu yawezayo kuleta uwiano katika maendeleo ya usalama wa nchi yetu. Asante. Nachangia na ninaunga."
}