GET /api/v0.1/hansard/entries/783366/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 783366,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783366/?format=api",
"text_counter": 198,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Obo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ambayo nimeitafuta kwa muda mrefu. Ningependa Wabunge wajue kwamba ukitetea askari wa eneo Bunge lako au jimbo lako, yule askari kesho atakuwa Lamu. Huwezi mlipa sawa askari aliye Nairobi na askari aliye Lamu katika Boni Forest. Huwezi ukamlipa sawa askari ambaye ako Gamba Police Station au Kiangwi na askari ambaye ako Nairobi. Tusitetee kwamba hao askari watabaki pale pale. Hawa askari kawaida wanahamishwa. Itakuwa si sawa. Itafika wakati askari watakataa kwenda kule. Kuna wengine wanakataa hata wako tayari kuacha kazi kwa sababu ya kupelekwa sehemu kama Lamu. Lazima wapewe posho---"
}