GET /api/v0.1/hansard/entries/783652/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 783652,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783652/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii ili nami pia niwaunge wenzangu mkono, kwamba tunahitaji halmashauri ya jiji la Nairobi, ili tupate usafiri wa kitaifa. Ukweli ni kwamba jiji la Nairobi ni letu sisi sote. Si la watu fulani. Ni la Wakenya wote. Jiji la Nairobi ndilo sura ya Kenya na pahali ambapo pesa nyingi ambazo zinatumika humu nchini hupatikana. Vile vile, nikiwapeleka nyuma kidogo kihistoria, ukiangalia wakati wa Rais Moi, utaona kwamba alijaribu kuweka usafiri kutumia mabasi ya Nyayo. Watu hawakumwelewa. Lakini leo hii, watu wakikaa, wanakumbuka kuwa Rais Moi alikuwa amefikiria kuwa na usafiri wa kitaifa. Rais Kibaki naye alitutengenezea barabara ya kwenda Thika na hata akataka kupanua barabara ya kuelekea Mombasa lakini siasa iliingizwa hapo. Nataka kuwakumbusha wenzangu: Kilio kilikuwa; kwa nini Nairobi? Sisi tunaoishi Nairobi tunajua matatizo yaliyoko Nairobi kuhusu usafiri. Ukweli ni kwamba Roma haikujengwa kwa siku moja. Ni lazima tuanzishe mahali kabla hatujaenda kwingine. Rais Uhuru Kenyata alivyoanza kazi yake, aliangalia kwa kina sana usafiri wa Mombasa hasa barabara ya Dongo Kundu, ambayo ilizungumziwa kwa muda mrefu. Sasa hivi inajengwa. Vile vile, barabara ya kutoka uwanja wa ndege inapanuliwa. Barabara ya kutoka Mariakani hadi Mazeras, ambapo kulikuwa na tatizo kubwa, inapanuliwa. Ukienda jiji la Kisumu, vile vile barabara zinapanuliwa. Tukubali Nairobi ikae hivi hivi na tuwe na matatizo milele ama Nairobi iwe ya kwanza kuangaliwa alafu huko kwingine kufuatie. Miaka iliyopita nikiwa Waziri niliwahi kusafiri kwenda Beijing, China. Nilikuta magari mjini ni zaidi ya milioni tano. Niliporudi baada ya miaka kadha, nilikuta wakijenga usafiri wa kitaifa. Nilipoenda tena niliuliza: “Haya imekuaje?” Sasa hivi, hakuna msongamano wa magari. Sasa usafiri wa kitaifa upo na watu wengi wanaowacha magari nyumbani na kusafiri kwa reli. Vile vile, Serikali ambayo inasimamia jiji la Beijing imeamua kuwa kuna siku ambazo magari fulani hayataruhusiwi mjini. Ukifika huko, unaona tofauti kubwa sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}