GET /api/v0.1/hansard/entries/783653/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 783653,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/783653/?format=api",
    "text_counter": 243,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Katika jiji la London, kuna usafiri mzuri sana. Serikali imewataka watu wasafiri na usafiri ule lakini wakati mwingine, watu wengine wanapendelea kuendesha magari yao na kwenda mjini. Wanalipa ridhia pesa nyingi wakiingia mjini bila sababu nzuri. Wanalipa karibu Kshs1,000 pesa taslimu za Kenya. Ukienda miji mingine mingi utaona kuwa kuna tofauti kubwa sana kupata usafiri wa kitaifa. Kuna wasiwasi kuwa kazi za Kaunti ya Nairobi zinachukuliwa na Serikali Kuu. Swali ni kuwa, je wakiachiwa, wataweza kutatua tatizo hili?” Ukweli ni kwamba haiwezekani. Kwa hivyo, ni lazima Serikali ya Kitaifa ifanye kazi na serikali ya kaunti ili kutatua matatizo haya. Mhe. Naibu Spika, Kenya yetu pale imefika sasa ni lazima tubadilishe. Tusiweke siasa katika kila kitu. Tubadilishe mwenendo. Tubadilishe kuwa miradi muhimu inayofanywa na Serikali ambayo inafaidisha Wakenya wote iweze kufanyika. Nafikiria tulikuwa na wewe hapa katika Bunge la Tisa. Wakati tukiwa hapa, kulizungumziwa sana upanuaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Ikaleta hisia mbaya na ikacheleweshwa mpaka sasa bei zilibadilika zikawa juu sana kwa sababu ya mradi ule kucheleweshwa. Ninawaomba wenzangu wajue kuwa jiji la Nairobi ni letu sote. Kila siku kuna pahali utaanzia na nina imani kuwa mwanzo ni Nairobi ili kwenda kwengine nchini Kenya kupanua usafiri wa maeneo yale. Jina hili la Nairobi linatia watu wasiwasi lakini ukweli ni kwamba suala hili lilianzishwa wakati wa wizara ya kusimamia masuala ya Nairobi. Ukienda nchi nyingi, utakuta kuwa miji mikuu ya nchi hizo yako na wizara ambayo inasimamia kila kitu. Hata ukienda Nigeria, Lagos ilishindikana na wakaenda Abuja. Wako na wizara inayosimamia masuala ya Abuja. Suala hili lilianzishwa na Raisi Kibaki wakati wa serikali ya mseto wakiwa na Waziri Mkuu kuwa kuna umuhimu wa kuwa na wizara ambayo inasimamia jiji la Nairobi. Sasa, kwa sababu wizara zimepunguzwa, haiwezekani kuwa na wizara ikisimama kivyake. Kuna umuhimu wa halmashauri hii iweze kusimamia masuala ya usafiri. Ndugu zangu na waheshimiwa wote, nawaomba tuunge mkono suala hili ili tuweze kuanzisha mradi huu ambao utaokoa hali ya usafiri na kuongeza hali ya uchumi. Pia, utawezesha wageni wanaokuja Kenya kutaka kuja zaidi na kuwekeza hapa ili watu wetu waweze kupata kazi. Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Naunga mkono."
}