GET /api/v0.1/hansard/entries/785626/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 785626,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/785626/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Didmus Mutua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1885,
        "legal_name": "Didmus Wekesa Barasa Mutua",
        "slug": "didmus-wekesa-barasa-mutua"
    },
    "content": "Kama Bunge la Kitaifa, tunapojiandaa na kujitahidi kupitisha huu Mswada, lazima polisi waanze kujipanga katika mafunzo na kwa kujua teknolojia za kisasa ili tupatie nafasi nzuri sheria hii. Nawarai Wabunge wenzangu tuipitishe kwa sababu ni sheria muhimu sana ambayo itahakikisha polisi na majasusi wetu wanatumia mbinu za kimataifa za kupambana na uhalifu wa teknolojia ambao umekua ukiongezeka kila wakati. Vile vile, naomba washikadau kwamba tunapopitisha hii sheria, lazima pia wawe wakitafuta mafunzo kutoka nchi ambazo zimeendelea kama Malaysia na Marekani ili kujua jinsi tekinolojia imewasaidia. Hiyo itatusaidia kupunguza uhalifu hapa nchini. Vile vile, ningependa kuchukua nafasi hii kuwaambia Wakenya ambao wamekuwa na mazoea ya kutumia teknolojia kwa njia ambayo haifai kwamba nafasi yao katika jela imefunguliwa. Sasa polisi watakuwa na nguvu ya kuwakamata. Wale ambao wanatukana wengine kupitia mitandao ya kijamii, wasifikirie kwamba hawawezi kukamatwa. Ninawaambia kwamba sheria hii ikipitishwa wajipange.Waache mazoea ya kutumia mitandao ya kijamii kwa minajili ya kutukana na kuwahangaisha wenzao. Sisi kama Wabunge tungependa jela zipunguzwe ili wahalifu wawe wachache. Hii ndio sababu ninatoa onyo kwa wakenya kwamba wajiepushe na mazoea ya kutumia mitandao ya kijamii kwa sababu hii sheria ikipitishwa, polisi watakuwa na ujuzi na nguvu ya kuwafuata na kuwakamata. Kwa hayo machache, naunga mkono. Ahsante."
}