GET /api/v0.1/hansard/entries/786102/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 786102,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/786102/?format=api",
"text_counter": 373,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "wanaitisha baadhi ya hivi vyeti ndiposa wapewe kazi. Tuko na maskwota katika eneo langu la Trans Nzoia. Hawa maskwota wanaishi maisha ya upweke; maisha wasiyoweza kupata pesa za kulipia watoto wao mahitaji yao. Hata ikija kwa upande wa kupewa vitambulisho, utaona vijana wetu pia wanaumia. Wao husema: “Leta pesa, nenda ujitambulishe unatoka wapi.” Inanyanyasa vijana wetu katika nchi yetu ya Kenya. Ndiposa Mhe. Sakaja, katika Bunge la Kumi na Moja, alileta Mswada. Tulifikiria kwamba watatekeleza mambo yaliyokuwemo katika Mswada ule lakini hayakutekelezwa. Kwa vile Mheshimiwa ameleta huu mjadala tena, nina imani utatekelezwa vilivyo. Nataka nigusie Huduma ya Vijana kwa Taifa. Vijana wamekosa nafasi kwa sababu wanaulizwa kuleta hizi stakabadhi. Tulileta Huduma Centres katika nchi ya Kenya ili kuondoa msongamano wa watu na kuhakikisha wanapata nafasi nzuri ya kuhudumiwa vizuri. Nina imani iwapo hii itatekelezwa, vijana wetu watapata nafasi nzuri ya kujimudu katika maisha yao. Najua uchumi wetu utaimarika tukihakikisha kuwa vijana wamekaa vizuri. Usalama wa nchi yetu hautakua mbaya. Vijana wetu hawataendelea kunywa pombe ama kutumia mihadarati. Naelewa kwamba kuna vijana wetu ambao wako kwenye vyuo vikuu ambao hawana baadhi ya hizi stakabadhi. Masharti ambayo yamewekwa hayawasaidii vijana kupata nafasi za ajira. Kuna baadhi ya ndugu zetu ambao wako kaskazini mashariki mwa nchi ambao wana miaka 40 ilihali hawajapata vitambulisho. Iwapo hii Hoja itapita, ninaomba Serikali ihakikishe imetekeleza yale vijana wetu wanataka."
}