GET /api/v0.1/hansard/entries/786215/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 786215,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/786215/?format=api",
    "text_counter": 96,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Senator Haji",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, namshukuru mwenzangu, Seneta wa Kaunti ya Siaya, kwa kuleta Mswada huu kujadiliwa katika Jumba hili. Pili, nawashukuru wote waliozungumza, husan ndugu yangu, Sen. Wetangula, kwa yale mambo mazuri aliyozungumza juu yangu. Bw. Spika, kama kuna mtu aliye na furaha kwa mwenendo uliochukuliwa na hawa viogozi wawili, ni mimi. Miezi michache iliyopita –nafikiri miezi mitatu au mine - nilimwita Sen. Wako na Sen. (Prof.) Ongeri na nikawaambia kwamba vile nchi inavyokwenda, itakuwa vibaya kama sisi, wazee na viongozi, hatutajishughulisha ili kuleta hawa viongozi pamoja. Hata hivyo, kwa bahati mbaya, tulipokuwa tukijaribu kutafuta wale ambao tungeweza kufanya kazi nao pamoja, wengine walitoa hiyo siri. Kwa hivyo, tuliona ya kwamba hatungeweza kuendelea na jambo hilo. Ilikuwa kisa kama vile Wazungu wanavyosema, “ letting the cat out of the bag.” The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}