GET /api/v0.1/hansard/entries/786218/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 786218,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/786218/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, viongozi hao wawili walisikizana Ijumaa, siku ambayo kwetu sisi Waislamu ni siku kubwa sana na ni siku muhimu kuliko zingine zote katika wiki. Tunaamini ya kwamba Mungu husikiza maombi ya siku hiyo. Kwa hivyo, naona kuwa Mungu amesikiza maombi yetu kwa kuwaleta hawa viongozi wawili pamoja. Bw. Spika, kama tulivyokaa hapa, tunavuta hewa ya matumaini ya kwamba Wakenya watakuja pamoja kuhakiksisha ya kwamba ule undugu ambao tumekaa nao kwa miaka yote hamsini, utakuja na kudumu zaidi. Kwa hivyo, tunawapongeza viongozi hawa wawili; Rais Kenyatta pamoja na Right Hon. Prime Minister, Raila Odinga, kwa kufanya walivyofanya. Tungependa kuuliza viongozi wote wa kisiasa, sio hawa wawili tu, twende pamoja. Ni lazima tuwaunge mkono kwa roho na kwa vitendo ili yale mambo waliyokubaliana yatekelezwe kwa njia itakayowasaidia wananchi wa Kenya. Bw. Spika, tulikuwa tumefika mahali ambapo hungelijua mtu ni wa Kabila gani. Wala hapakuwa na haja ya kuuliza kuhusu kabila. Hata hivyo, katoka mwaka wa 2007, watu walianza mambo ya kutengana na hali ikawa mbaya zaidi katika uchaguzi wa juzi. Sisi viongozi tuko hapa na tumechaguliwa na watu ambao wanangoja tuwaonyeshe mfano mzuri. Kwa hivyo, tunafaa kuwashukuru hawa viongozi wawili kwa kutuonyesha mfano mzuri. Bw. Spika, nataka kuwauliza Maseneta katika Jumba hili la ‘wazee;’ ambapo labda mimi ndiye mzee zaidi, ingawa tunashindana kwa umri na Sen. (Prof.) Ongeri."
}