GET /api/v0.1/hansard/entries/786260/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 786260,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/786260/?format=api",
    "text_counter": 141,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa nafasi. Siku ya Ijumaa ni siku muhimu sana haswa kwa jamii ya Waislamu lakini viongozi hao wawili sio Waislamu. Cha kushangaza ni kuwa walikutana siku ya Ijumaa na Mwenyezi Mungu aliibariki siku hiyo. Nachukua nafasi hii vilevile kuwapa kongole kwa ujasiri wao kukutana licha ya kuwa walikuwa wapinzani. Kuna baadhi ya Wakenya waliopoteza maisha yao kutokana na vita. Nina furaha kwamba Kiongozi wa Wachache katika Seneti alieongea na sikuona mtu yeyote upande ule mwingine akitoa hoja ya nidhani na hiyo si kawaida. Natumai kuanzia leo hoja za nidhamu hazitakuepo. Jambo la muhimu ni kwamba sote twahitaji amani katika nchi ya Kenya. Bibilia pia inatuhimiza kupenda jirani zetu kama tunavyopenda nafsi zetu. Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu. Jukumu letu sisi kama Wakenya ni kuona kwamba Kenya yetu inaendelea mbele kimaendeleo na kiuhusiano."
}