GET /api/v0.1/hansard/entries/786287/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 786287,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/786287/?format=api",
"text_counter": 168,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nimesimama kuunga mkono Hoja ya Sen. Orengo na kuwapongeza viongozi wetu,vinara wawili; Mhe. Rais Uhuru Kenyatta na Mhe. Raila Amollo Odinga. Viongozi hawa walikuwa mahasimu wajadi lakini juzi, siku tukufu ya Ijumaa, walikuja pamoja, wakakumbatiana, wakapeana mikono na wakashusha hali mbaya ya siasa ambayo iliyokuwepo katika nchi yetu ya Kenya. Ilhali, yapo mengi ambayo bado yana takikana kufanywa kwa sababu ukabila, ufisadina mambo mengi ambayo waliyazungumzia bado yako. Ni lazima tushirikiane kama Bunge la Seneti na nchi kwa jumla kuhakikisha kwamba yametatuliwa. Jambo moja ambalo ningependa kuzungumzia ni kwamba hatuna kitu cha kutuunganisha pamoja sisi kama Wakenya kwa sababu kila mtu akitoka katika Bunge hili la Seneti, ana kwenda katika kabila lake. Zamani, tulikuwapo na redio ya kitaifa, idhaa ya taifa; Sauti ya Kenya, lakini sasa, kila mtu anaskiza redio ya kabila lake. Hiyo ni mbaya kwa nchi hii kwa sababu hatuna kitu ambacho kina tuunganisha kama Wakenya. Kuna wakati hayati Mwalimu Nyerere alizungumzia kabila akasema kwamba katika Karne ya 21, hakuna mtu anatakikana kupanda basi ya kabila. Ukabila ulikwisha kwa sababu watu wa Ulaya walijiunga pamoja na kuwa European Union. Sisi tumejiunga pamoja kama East African Community, lakini bado tunarejea katika makabila yetu ili kuwahujumu wengine. Kwa hivyo, tutafute kitu ambacho kitatuunganisha pamoja kama Wakenya. Hii itakuwa ni lugha ya Kiswahili ambayo tunaitumia kama lugha ya taifa. Kwa sababu kama hatuna kitu cha kutujumuisha pamoja kama Wakenya, yale yote yanayofanywa hapa yatakuwa ni ya bure. Yaliyofanyika mwaka wa 1997, 2007 na 2017 yanaweza kufanyika tena kama hatutakuwa na mambo ya kudumu ya kuondoa ukabila. Kwa hivyo, ni lazima tulete taasisi ambazo zitahakikisha kwamba kuna usawa, hakuna ukabila na zitaondoa ufisadi ili kuhakikisha kwamba nchi yetu ya Kenya inasonga mbele. Kwa hayo mengi, Bwana Naibu Spika, naunga mkono Hoja ya Seneta Orengo. Asante."
}