GET /api/v0.1/hansard/entries/786289/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 786289,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/786289/?format=api",
    "text_counter": 170,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "March 14, 2018 SENATE DEBATES 30 Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Nataka kuunga mkono Hoja hii. Kwa kweli, hakuchi, hakuchi, hatimaye kumekucha. Nasema hivi kwa sababu hawa viongozi wawili tayari wamesalimiana na wakasema kwamba Kenya ni moja na msukumo wa mambo ambayo yametuunganisha hayawezi yakatenganishwa. Kwa hivyo, sisi kama viongozi hapa Seneti, tunawaunga mkono na kusema kwamba lile walilofanya ni jambo la umuhimu sana. La kufanya sasa ni kuhakikisha tuko na taasisi muhimu; na zile tulizo nazo, tuzitilie nguvu. Tukifanya hivi, tutahakikisha kwamba yale mambo yaliyozungumzwa yasiwe tu maneno makavu, bali yawe mambo yatakayo kuwa vizuri katika Katiba yetu. Vile vile, hatutaki iwe katika Katiba yetu peke yake, bali pia iwe katika mioyo na mawazo ya Wakenya. Bwana Naibu Spika, baada ya wale viongozi wawili kusalimiana siku ya Ijumaa, madaktari wengi kutoka sehemu nyingi za Kenya wameniambia kwamba wagonjwa waliokuwa wakitembelea zahanati zao wamepungua. Hii ni kwa sababu kulikuwa na hali ya taharuki na sintofahamu katika nchi yetu. Lakini sasa, baada ya hawa viongozi wawili kusalimiana, inaonekana kuwa umoja na undugu umeimarika katika nchi yetu ya Kenya. Langu ni kusema kwamba ikiwa hali hii itaweza kuendelea hivyo mpaka mwaka wa 2022 na 2027, basi itakuwa vizuri kwa Wakenya wote. Lakini inafaa ijulikane vizuri kwamba lile jambo linalotuogofia lisiwe tu ni siasa, bali ionekane ni siasa na iendelee kuwekwa katika taasisi zetu ambazo zitaaminika sasa na hata baadaye. Asante sana, Bwana Naibu Spika."
}