GET /api/v0.1/hansard/entries/78806/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 78806,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/78806/?format=api",
"text_counter": 532,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii, na pia kuruhusu swala hili lizungumziwe kwa kirefu. Jambo la kusikitisha hapa nchini ni kuwa haswa wale ambao ni wanyonge ndio wanazidi kunyongolewa mbali. Ni makosa sana kwa Wakenya ambao ni wadogo kwa idadi ama sio wengi katika Serikali kuonewa namna hii. Si bwana huyu tu ambaye ameharibiwa maisha yake kwa sababu ukitaka kumumaliza mtu, mnyime mbegu zake za kupata watoto na pia maisha yake na utakuwa umemmaliza yeye na vizazi vyake vyote. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni jambo ya kusikitisha na huzuni sana kuwa miaka 47 baada ya kupata Uhuru, Wakenya bado wanatesana namna hii. Ni jambo la kusikitisha kuwa sasa hivi tuko na ukoloni mamboleo badala ya ukoloni ule ambao ulikuweko tukipigania Uhuru. Ukiangalia sana, jambo la kusikitisha haswa ni kuwa jamii ya Wasomali na pia waislamu kwa ujumla Kenya hii hawana faida. Kwa sababu hawana faida, wanateswa, wanashikwa na kupelekwa Uganda na kufanywa mambo mengi ya ajabu ajabu kwa sababu wao hawatakikani kuwa kama Wakenya na kufurahia matunda ya Kenya hii, haswa wakati huu ambao tumepitisha Katiba mpya. Haki zao za kibinadamu zinachezewa na kila mtu. Haswa ikiwa chifu anateswa hivyo, hao wengine wanaweza kufanywa vipi? Tunasikitika sana siku ya leo. Haswa nakumbuka vile malalamishi yalivyofika hivi leo, wengine wetu tulishika matumbo kwa uchungu kwa sababu tulishangaa ni nani huyo anayeweza kuwafanyia wenzake kitendo cha kinyama namna hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni lazima sisi kama Serikali tuchukue jukumu la kuhakikisha kuwa Wakenya wanaishi kwa amani na kufurahia haki yao ya kuwa Wakenya haswa wakati huu baada ya kupitishwa kwa Katiba mpya. Bw. Naibu Spika wa Muda, naunga wenzangu mkono kuwa jambo hili lazima likomeshwe sasa hivi."
}