GET /api/v0.1/hansard/entries/788173/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 788173,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/788173/?format=api",
    "text_counter": 209,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadime",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, mazingira yameharibika. Ile mvua tulikuwa tunapata zamani haipo tena. Mtu anapoongea juu ya unyunyizaji maji wa mashamba, huo ni mwelekeo mwema. Mwenyezi Mungu, kabla hajatuumba sisi binadamu, alitupatia maji, hewa na chakula. Vitu vingine kama vile nguo na usalama yalikuja baadaye. Ukimpa binadamu chakula, utakuwa umempa maendeleo. Ukifananisha nchi yetu ya Kenya na nchi zingine, utakuta kwamba Mwenyezi Mungu alitupa ardhi nzuri ambayo ina rotuba nyingi. Shida ni kwamba mipangilio yetu haiko sawa sawa. Yule aliyeleta huu Mswada kuhusu unyunyizaji maji sharti tumpe kongole. Kule kwangu katika Kaunti ya Taita, Eneo Bunge la Mwatate, kuna milima mingi. Mikondo ya maji pia ni mingi. Kila wakati maji ya mvua yanabomoa nyumba za watu. Maji hayo huwa mengi kiasi cha kuathiri wananchi. Tungekuwa tunatengeneza mabwawa ama c heckdams, basi tungewasaidia wananchi pakubwa sana. Hayo maji yaliyohifadhiwa yanaweza kutumika na wafugaji kwa mifugo yao na hata yakanywiwa na watu. Aidha yatatumika katika unyunyizaji maji kwa mashamba na mambo mengine mengi. Rotuba ya Taita Taveta na Mwatate kwa ujumla ikipata maji inaweza kulisha Kenya nzima. Maji tu ndiyo tatizo kubwa. Wananchi sasa hivi wanashindana na wanyama kwa sababu ya maji. Nakumbuka mwaka juzi, Februari, tulipoteza watu kumi na wanane kwa sababu ya kutumia maji yaliyokuwa na madhara. Kule kuna madini. Ukichimba kisima utagundua kwamba maji yake yana madini. Baada ya muda mrefu, wananchi wanaokunywa hayo maji hupatikana na matatizo. Mabwawa yakitengenezwa, yatasaidia sana. Yale maji ambayo huelekea baharini tutayahifadhi. Lakini yakizuiliwa itakuwa vizuri. Kama unavyofahamu, kule kwetu Taita Taveta ndiyo eneo pekee hapa Kenya ambayo ni disease free zone . Hata watu ambao wanalisha ng’ombe wakitaka kuziuza wanazileta huko kwetu. Lakini, maji ni tatizo kwetu. Tukiwa na mabawa jimbo letu litakuwa na maendeleo mengi na kwa jumla litasaidia Kenya nzima."
}