GET /api/v0.1/hansard/entries/788687/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 788687,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/788687/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Katana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 691,
        "legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
        "slug": "aisha-jumwa-katana"
    },
    "content": "ambayo inaangalia masuala ya kuzuia, kuthibithi na matibabu katika taifa letu la Kenya. Lakini sheria kama hizi zimepewa kisogo na Serikali. Hazipewi kipau mbele na hazina ufadhili wa kutosha wa kuziwezesha kulishughulikia suala la kukinga, kuthibithi na hata kutibu saratani. Vipengele vya 4 na 20 vya sheria hii…. Ni vyema sisi kama Wabunge ambao tunaadhiriwa na jambo hili moja kwa moja kwa kuhusika katika michango kusaidia wagonjwa katika maeneo yote kwa njia moja ama nyingine ili wapate matibabu... Majibu tunayoyapata baadaye si ya kuridhisha. Mara vifo vinatokea wakati tumechanga pesa zetu kiasi ili mgonjwa apate matibabu. Ndio maana nataka nimpongeze Mhe. Waruguru. Kuna umuhimu wa kuwa na hazina ili itumike mashinani kwa kuhamasisha jamii na hatimaye watu wakijua hali yao mapema, maana Shirika la Afya Ulimwenguni linatuambia kuwa saratani ikijulikana mapema inaweza kutibithiwa na kutibiwa. Kwa hivyo, kupatikana kwa ufahamu wa mapema ni jambo la muhimu."
}