GET /api/v0.1/hansard/entries/788712/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 788712,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/788712/?format=api",
    "text_counter": 253,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chelule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13126,
        "legal_name": "Liza Chelule",
        "slug": "liza-chelule"
    },
    "content": "Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo inaongea juu ya saratani. Saratani ni ugonjwa ambao imetatiza wananchi wote. Hatusemi huu ni ugonjwa unaoadhiri eneo Bunge moja na haiadhiri nyingine. Tunaelewa wananchi wameumia sana kwa sababu ya ugonjwa huu. Ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza Mbunge ambaye ameleta Hoja hii ili tujadiliane na tukubaliane kama Wabunge kuwa ugonjwa huu unafaa kutengewa pesa. Umma unahitaji kuelimishwa juu ya ugonjwa huu kwa sababu ni ugonjwa ambao, ukijulikana kwa wakati mzuri, unaweza tibiwa na mtu apone. Shida kubwa ni kuwa ni ugonjwa ambao unapata watu pale nyumbani, vijijini na mijini. Ugonjwa huu ukipatikana kwa wakati mzuri, unaweza kutibiwa. Ikipatikana kwa wakati uliyochelewa, huwa kwa kawaida unatatiza wananchi sana. Watu wengi wameuza mali yao na wakapata shida nyingi sana kwa sababu ya saratani. Tunapoongea sasa hivi, kuna watu ambao wamelala hospitalini na wengine nyumbani na wengine wameshindwa na matibabu. Kwa hivyo, ni vyema Serikali itilie maanani kwa kutenga pesa kwa ugonjwa wa saratani. Kwanza ni muhimu kuwe na elimu ya umma kuhusu ugonjwa huu. Pili, ni muhimu kupeleka huduma hizi vijijini ili wananchi wachukue wakati wao kwenda kupimwa ndio ijulikane kwa wakati unaofaa. Mtu akipatikana nayo, iwe ni kwa wakati unaofaa, wakati wanaweza kupata matibabu na wapone. Naunga mkono Hoja hii, na pia Mbunge aliyeileta. Nina hakika kuwa Wabunge wote wataipitisha na kuhakikisha kuwa Serikali imetenga pesa kwa sababu ya Hoja hii. Ni ya maana sana na sisi sote tutafurahi. Ni jukumu letu kama viongozi kuelimisha wananchi kwa kutumia njia yoyote ili kuhakikisha kuwa watu wamepata elimu na wamepimwa kwa wakati unaofaa ili wapate matibabu."
}