GET /api/v0.1/hansard/entries/789450/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 789450,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/789450/?format=api",
"text_counter": 87,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante sana, Bwana Spika kwa kunipa fursa hii kujiunga na Wakenya wengine na wakaazi wa Murang’a kuomboleza kifo cha hayati Matiba. Sisi watu wa Pwani, tulimtambua Matiba kama mwekezaji mkubwa katika biashara ya utalii katika eneo la Pwani. Vile vile, alikuwa rafiki mkubwa wa Pwani kwa sababu wakati alipokuwa akiwaania kiti cha Kenya Football Federation (KFF) kama mwenyekiti, Pwani ndio ilimuunga mkono wa kwanza ndiyo nchi nzima ikafuata badaaye. Kwa hivyo, tunamtambua hayati Matiba kama kiongozi ambaye alikuwa akiwapa kipaumbele Wakenya ambao hawakubahatika kijamii, aidha kimasomo, kibiashara na katika hali zingine za kijamii. Kifo cha Matiba pia kinatukumbusha wale wengine ambao walitangulia kufa kama vile marehemu Salim Ahmed Bamahriz ambao walikuwa pamoja naye katika chama cha Forum for the Restoration of Democracy (FORD) Asili wakipigania uhuru wa pili wa nchi ya Kenya. Kwa sasa, sisi kama Wakenya, jambo la kusikitisha ni kwamba bado tunayapata yale mambo ambayo Matiba alipigania katika nchi yetu ya Kenya. Kwa mfano, mambo kama kura kuibiwa na watu kuuawa kiholela wakidai haki zao bado yanaendelea kufanyika katika nchi ya Kenya. Haya ni kinyume cha yale malengo ambayo Matiba na wenzake walipigania wakati tulipopigania uhuru wa pili. Kwa hivyo, bado tuna safari ndefu sana ya kupigania haki yetu katika nchi hii kuhakikisha kwamba tumepata uhuru kwa Wakenya, hasa wale wadogo ambao hawakubahatika kuwa na fursa za kibiashara ama za elimu kama wale wengine ambao wako katika mamlaka. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}