GET /api/v0.1/hansard/entries/789452/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 789452,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/789452/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, Bwana Spika, tunapoendelea kuomboleza, tunaomba kwamba sisi kama Wakenya, hasa viongozi ambao wako sasa, ni lazima tuangalie ile njia ambayo tumetoka na tujue makosa yalifanyika na vile tunaoweza kuyaepuka kwa siku za mbele. Tunapaswa kufanya hii hasa kwa wakati huu ambapo kuna msukosuko katika taasisi yaIndependent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) . Tunafaa kuanza mwanzo mpya kuhakikisha kwamba nchi yetu ya Kenya imewekwa katika msimamo ambao utakuwa na matumaini kwa Wakenya wanaokuja siku za usoni. Asante sana, Bwana Spika."
}