GET /api/v0.1/hansard/entries/790664/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 790664,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/790664/?format=api",
    "text_counter": 145,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Obo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Haya yanatokea zaidi kule Lamu kwa maafisa wa Serikali. Kwa mfano, polisi wakikaa pahali kama Kiunga kwa muda mrefu, wanasumbuka akili hadi wengine hutatizika kwa utenda kazi wao. Wanasumbua wananchi kusudi washtakiwe ili wapate faida ya kutolewa mahali hapo kwa sababu wamekaa kwa muda mrefu, kwa mfano, miaka saba. Wanahitaji ushauri nasaha ili wasaidike. Hata walimu wanahitaji huduma hizi. Walimu wanaofanya kazi kule Kiongwe, Boni Forest, wanastahili wapate huduma hizi kwa sababu sehemu hii ni ya kutisha. Inawasumbua akili hadi familia zao zinatatizika. Saa nyingine wanafanya vitendo vya kushangaza hadi unajiuliza kama wao ni binadamu au la. Kumbe huwa ni matatizo yanayotokana na ile hali wako nayo kule Lamu."
}