GET /api/v0.1/hansard/entries/790707/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 790707,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/790707/?format=api",
    "text_counter": 188,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Tayari",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13379,
        "legal_name": "Benjamin Dalu Stephen Tayari",
        "slug": "benjamin-dalu-stephen-tayari-2"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia mjadala huu kuhusu mambo ya uandikishaji wa vitambulisho na stakabadhi za kuzaliwa. Kusema ukweli, mwanzo katika eneo Bunge langu, hii ni shida sugu sana. Wananchi wanapata taabu sana kupata huduma hii ambayo ni muhimu sana katika nchi yetu. Utaona ya kwamba sanasana vile tuko na shida za barabara wananchi wanatoka kilomita nyingi ili kufika kwenye vituo ambavyo viko Kinango peke yake. Mwananchi anatumia siku nzima ili kupata huduma kama hii. Kwa hivyo, mimi naunga mkono mjadala huu kwamba ni lazima Serikali ijaribu kuangalia ya kwamba hii huduma inasambazwa katika vituo vidogo vidogo, sana sana kwa ofisi za machifu. Pia vifaa vitolewe kwa wingi ili wananchi waweze kupata huduma hii. Hivi sasa tunatumia pesa yetu kutoa pesa ya mafuta kupatia wale wafanyikazi ili waende wakaandikishe wananchi. Pia tunavyojua hivi sasa kama hana cheti cha kuzaliwa mwanafunzi haandikishwi katika shule yoyote. Na wanafunzi wengi sana hawana hivi vyeti. Ikiwa ni lazima wasafiri kutoka maeneo mbalimbali kuenda kupata hii huduma, ni njia ambayo itatatiza sana wananchi. Kwa hivyo mjadala huu utatusaidia sana. Ningependa kuomba utiliwe mkazo sana kwa sababu tuko katika hali ambayo tumengojea kwa siku nyingi sana. Wananchi wasipate taabu kufuata huduma hii. Pia tunaona ya kwamba teknolojia ambayo imefika sio lazima mwananchi atembee mbali. Ni kitu kidogo sana ambacho kinaweza kufanywa kutumia teknolojia ili wananchi wapate huduma hii. Kwa hivyo nashukuru sana kwa muda huu na ninaunga mkono mjadala huu. Asante sana."
}