GET /api/v0.1/hansard/entries/790732/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 790732,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/790732/?format=api",
    "text_counter": 213,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii ili nichangie Hoja hii. Kwanza, naunga mkono Mhe. Martha Wangari kwa kuleta Hoja hii muhimu sana kwa maisha ya wananchi wa Kenya. Ametoa mfano mzuri wa mahali kama Gilgil ambako watu wanasongamana sana huko Naivasha. Amesema kwamba alipofika hapo aliona watu takribani mia tano ambao walikuwa wameketi kwenye ofisi za usajiri."
}