GET /api/v0.1/hansard/entries/790733/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 790733,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/790733/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Naunga mkono Hoja hii kwa sababu itawawezesha watu wengi hasa akina mama kusajili watoto wao ndiyo waingie shuleni. Siku hizi ni sheria kwamba kila mtoto ama mwanafunzi lazima asajiriwe na stakabathi ya kuzaliwai ili aweze kuingia shuleni. Vile vile, natoa pendekezo kwa Serikali kwamba wakati hawa watoto wote wanaingia shuleni wanakuwa na stakabathi za kuzaliwa ambazo zinaonyesha wao ni Wakenya. Moja kwa moja wakimaliza shule wapewe vitambulisho vyao haraka iwezekanavyo ili wakitoka shuleni hakuna haja tena kuzunguka ofisi mbalimbali ili kupewa stakabathi hii muhimu."
}