GET /api/v0.1/hansard/entries/790734/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 790734,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/790734/?format=api",
    "text_counter": 215,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Tumeona watu wakienda sehemu mbalimbali kutafuta stakabathi hii na maofisa wa Serikali wakati mwingine wanachukua advantage yao kwa sababu wana hamu ya kupata stakabathi hizi. Kwa hivyo, wanafanya ufisadi na hii si haki. Lakini hii huduma ikienda katika Nyanja, kwa mfano kutoka kwenye eneo bunge mpaka wadi, litakuwa jambo la maana sana. Huduma hii itakuwa imerushwa nyanjani na watu wetu watasaidika kwa haraka. Tunaona kuwa wengi hawawezi kutafuta kazi ikiwa hawana vitambulisho. Wengi katika kutafuta stakabadhi za kuonyesha umiliki hawawezi kumiliki mali zao bila kupata vitambulisho kama Wakenya. Kuwezesha na kuona kuwa huduma hii inapatikana kwa njia nyepesi kutarahisisha na kuona kuwa wananchi wetu wanapata huduma hii haraka iwezekanavyo. Jambo ambalo ningependa kusisitiza ni kuwa watoto ambao wanasoma katika shule zetu ni Wakenya. Kuwalazimisha watoto wale kuonyesha na kwenda na stakabadhi za kuzaliwa shuleni kunarahisisha kazi ya kuwapa vitambulisho kwa haraka iwezekanavyo ili kujitafutia hali yao ya maisha na vilevile kujisaidia katika kumiliki mambo mengi katika nchi hii ya Kenya. Tumeona katika sehemu mbalimbali kumekuwa na matatizo makubwa sana kwa sababu ya miundo msingi ambayo iko. Watu wanatembea mwendo mrefu ili kupata huduma hii. Ni muhimu kwa Serikali pia kuzingatia miundo msingi katika sehemu ambazo watu wanaenda kupata huduma kama hii. Nachukua fursa hii nami kumuunga mkono Mhe. Martha kwa Hoja aliyoileta na vilevile kukushukuru kwa kunipatia fursa hii kuchangia. Asante sana."
}