GET /api/v0.1/hansard/entries/790749/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 790749,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/790749/?format=api",
"text_counter": 230,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Mizighi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13274,
"legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
"slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
},
"content": "Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii hata mimi nichangie Hoja hii ambayo ni ya muhimu sana kwetu sisi, haswa akina mama. Zoezi hili la kutafuta vyeti vya kuzaliwa vinatuhusu sana. Nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Martha kwa kuifikiria Hoja hii na kuileta hapa Bungeni ili tuweze kuijadili. Ni kweli, mambo ya kutafuta vyeti vya kuzaliwa vimekuwa kero kwa wananchi wote wa Kenya. Ni shida sana. Wananchi wanasafiri mbali, wanaenda wakirudishwa, wanatumia pesa nyingi na kila wakifika pale, wanaambiwa warudi siku inayofuatia. Hivi majuzi, kule kwetu Taita Taveta, hata yale makaratasi ya kuchapisha vyeti hivyo hayakuwepo. Kwa hivyo, ilikuwa ni usumbufu mtupu wa kungoja. Pia, watoto wakienda shuleni wanaambiwa ni lazima wapeleke vyeti hivyo. Imekuwa ni kero sana manake vyeti ni muhimu. Huwezi kupata pasi ya kusafiri mpaka uwe na cheti cha kuzaliwa. Kwa hivyo, naunga mkono kwamba Hoja hii ni muhimu na tunaomba vyeti hivi viweze kupatikana kwa urahisi. Tunaomba huduma hii ya kutoa vyeti vya kuzaliwa iweze kuboreshwa na iwe rahisi kwa wananchi kuvipata vyeti hivi. Kama vinaweza kuletwa kwa ward level itakuwa vizuri zaidi. Nazidi kumpongeza dadangu Martha kwa kuileta Hoja hii Bungeni ili tuweze kuwasaidia wananchi kule mashinani."
}