GET /api/v0.1/hansard/entries/790758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 790758,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/790758/?format=api",
"text_counter": 239,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Asha Mohamed",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13262,
"legal_name": "Asha Hussein Mohamed",
"slug": "asha-hussein-mohamed"
},
"content": "Kwa sababu ya umaskini, kuna wazazi wengine hawana pesa ya kulipa stakabadhi ya kuzaliwa kwa watoto wao. Wanapozaa ndani ya nyumba, hawaendi kuandikisha watoto wao. Kuna wazazi wengine ambao wanapeleka watoto kliniki. Baada ya muda wa miezi tisa ama mwaka mzima wanamaliza kliniki, kulingana na yale makaazi nyumbani, wale wazazi wanapoteza zile kadi za kliniki. Unapokwenda kujiandikisha, ni lazima uwe na stakabadhi ya kuzaliwa kwa mtoto na kadi ya hospitali ya chanjo. Kuna ndoa za mapema: Utakuta mtoto anazaa mtoto. Wakati wakuchukuwa hii stakabadhi, inagundulika kwamba mama hana kitambulisho ambacho kinahitajika ili kusajili mtoto aliyezaliwa. Kunao wajane na wale single mothers ambao huambiwa wapeane kitambulisho cha baba ya mtoto. Wanalazimika kwenda kwa wakili ili waape. Hayo yote yanawagharimu senti."
}