GET /api/v0.1/hansard/entries/791950/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 791950,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/791950/?format=api",
    "text_counter": 104,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Pukose",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1458,
        "legal_name": "Robert Pukose",
        "slug": "robert-pukose"
    },
    "content": ". Hoja hii ambayo inasema kuwa kitambulisho na cheti cha kuzaliwa vipeanwe katika eneo Bunge ama sub-county ni jambo muhimu ijapokuwa nitaikosoa tu kwa sababu inasema “ urges” badala ya kusema “ resolves” . Bunge lina uwezo wa kuamua kwamba vyeti vya kuzaliwa na vitambulisho vipeanwe katika maeneo Bunge ili iwe rahisi kuvipata. Nakumbuka wakati wa kwanza vitambulisho kupeanwa. Hiyo picha ilikuwa inachukuliwa baada ya kuchukuliwa alama za vidole na unapewa kitambulisho hapo. Mtu akihitaji cheti cha kuzaliwa, anakuja Nairobi na inachukua muda kutengenezwa. Mwananchi anapewa kitambulisho ama cheti cha kuzaliwa baada ya mwezi mzima ama miezi miwili. Wakati mwingine anaambiwa makaratasi ambayo alijaza yalipotea. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa Muda, hili ni jambo ambalo Bunge hili linapaswa kufanya uamuzi mwafaka ili kuhakikisha kwamba vitambulisho na vyeti vya kuzaliwa vinapeanwa katika maeneo Bunge, badala ya wananchi kusafiri hadi Nairobi. Kwa hivyo, hii ni Hoja nzuri ambayo naiunga mkono. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda."
}