GET /api/v0.1/hansard/entries/796736/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 796736,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/796736/?format=api",
"text_counter": 733,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii. Jambo la kwanza kabisa, kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kuzungumza hapa Bungeni ni kuwashukuru watu wa Galole kwa kunichagua. Pili, kwa sababu ya muda, vile unavyojua Kaunti ya Tana River kila wakati kuna janga la mafuriko ama ukame. Shida imetupata huko Tana River na imetuathiri sana. Hivi sasa, asilimia sabini ya kaunti yetu iko ndani ya maji. Nilitoka huko jana na watu wengi katika eneo Bunge langu katika wodi za Wayu, Mikinduni, Chewani na Kora wako ndani ya maji. Hivi sasa, watu wamezungukwa na maji na watu kumi na nne hawajulikani waliko. Kuna sehemu nyingi ambazo barabara pia zimeharibika. Tumepewa chakula kidogo na Serikali lakini hatujui vile chakula hicho kinaweza kuwafikia walioathirika. Tumepewa chopper na Serikali lakini imeharibika. Mpaka sasa watu wako kwa shida. Kwa hivyo, tunaomba kitengo cha Serikali kilichopewa nafasi hii wasaidie sehemu zilizoathirika katika kaunti ya Tana River. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}