GET /api/v0.1/hansard/entries/796919/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 796919,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/796919/?format=api",
    "text_counter": 71,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadime",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Kwa kweli, haya malalamishi yanaenea kila mahali. Nikiangalia katika barabara ambayo imetengenezwa na KeNHA kutoka Voi mpaka Taveta, kuna watu wengi sana katika sehemu za Mlughi, Bura na Chavia, ambao hawajapata fidia licha ya kwamba ujenzi wa barabara hiyo ulikamilika zamani. Watu wengi kule Mwatate wanataabika kwa sababu hawajui wataenda wapi. Kila wakati wanakuja kwangu. Kila ninapoenda katika ofisi ya mashamba ninapata watu hao hawajalipwa fidia. Wengine wamepata fidia na tunashukuru, lakini wengine hawajapata. Naiomba Kamati ijaribu kuangalia wakati hizi barabara zinatengenezwa ndio angalau tusiwache hao watu wakiumia kwa sababu ni binadamu kama sisi."
}