GET /api/v0.1/hansard/entries/797265/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 797265,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/797265/?format=api",
"text_counter": 417,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": "Asante Bwana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii. Nasimama kumpa kongole Mheshimwa Rais kwa Hotuba aliyotoa jana. Lakini pia nasikitika kuwa watu wa Tana River, wakati Mheshimiwa Rais alizungumza kuhusu masuala ya barabara katika maendeleo, walitarajia awatajie kuwa barabara ya Tana River, ambayo ilianza kujengwa nikiwa darasa la tatu itajengwa. Miaka 50 tangu tupate Uhuru, hatuna barabara nzuri. Juzi nikitoka Bura nikienda Garissa upande wa Madogo, ilibidi niogelee katika mashimo saba kwa hiyo barabara iliyokatika. Inasikitisha sana. Mheshimiwa Rais ako na mipango mizuri kwa Wakenya lakini baadhi yetu, ufisadi umetufanya hatuhurumiani. Nashukuru waliotoa Hoja ya Fedha za Kusawazisha kwa sababu huko kwetu, baadhi yetu tunaishi ni kama tuko nchi nyingine. Sisi si Wakenya kama wengine. Hatuna barabara mashinani. Hata barabara kuu hatuna. Hatuna hospitali. Ikiwa pesa za kusawazisha maendeleo zitapatikana, zitaokoa baadhi yetu kwa sababu hali yetu ni ya kusikitisha, hasa watu wa Tana River."
}