GET /api/v0.1/hansard/entries/797811/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 797811,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/797811/?format=api",
    "text_counter": 185,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niangazie mambo machache katika hotuba ya Mhe. Rais Uhuru Muigai Kenyatta. Ninaiunga mkono kwa sababu ililenga kuunganisha wananchi wetu wa tabaka mbalimbali; maskini na matajiri na wale ambao wana milengo tofauti ya kisiasa. Jambo la kufurahisha muno tuliaona viongozi wetu wakisalimiana kuashiria umoja wetu. Kwa hivyo, ninamuunga mkono kwa dhati katika jitihada zake za kuwaunganisha Wanakenya wote bila ubaguzi wowote Pia ningependa kumuunga mkono Rais wetu katika maswala yake manne makuu ya kimaendeleo aliyoyaangazia katika hotuba yake. Wakati huu tunayafanyia kazi maswala haya manne makuu ili tuweze kuwa na maendeleo katika nchi yetu. Ninamuunga mkono katika vita vyake dhidi ya ya ufisadi ambavyo aliviangazia vizuri katika hotuba. Alisema yuko tayari kupigana na ufisadi hapa nchini. Hata hivyo, nina masikitiko mengi kwa vile hakuzungumzia maswala mengi ambayo niliyatarajia ayataje katika hotuba hiyo. Kwa mfano, swala la mafuriko ni swala nyeti wakati huu hapa nchini, hasa Kaunti ya Tana River. Ninapozungumza sasa hivi, zaidi ya vijiji 30 vimezama huko Kaunti ya Tana River. Shule kadhaa hazijafunguliwa mpaka leo hii. Watu wametoka katika sehemu zao za makazi na kwenda kuishi kwingine. Mali imeharibika. Mimea kama vile mahindi, maharagwe, na kadhalika yamesombwa na maji. Watu wa Tana River wamo hatarini ya kupata magonjwa yanayotokana na maji machafu. Maji haya yanatiririka kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Kwa hivyo, mimi kama Seneta wa Kaunti ya Tana River ambako kuna mafuriko mengi, nilitarajia Mhe. Rais Uhuru kulizungumuzia swala hili na kulitangaza kama janga la kitaifa na juhudi zaidi zifanywe ili kuwasaidia watu wetu. Ni lazima tuliangazia janga hili kwa undani zaidi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}