GET /api/v0.1/hansard/entries/797813/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 797813,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/797813/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, vijiji ambavyo vimezama katika Kaunti ya Tana River, hasa maeneo ya Tana Delta ni zaidi ya 30. Watu waliokuwa wanaishi humo wamehamia sehemu zingine. Hali hiyo inatatanisha kabisa. Tunajua kuna shida ambayo inaweza kungojea kesho au kesho kutwa, lakini shida ya Tana River ni mbaya; haiwezi kukongojea jioni, kesho au kesho kutwa. Shida hiyo inafaa kushughulikiwa mara moja. Hi ni kwa sababu watoto wetu hawaendi shule kutokana na mafuriko hayo. Shule chache ambazo zimefungulilwa, wanafunzi hawawezi kufika kwa sababu kuna maji mengi sana ambayo yametenganisha shule na makazi ya watu. Ni vigumu kufika katika vituo vya afya na kupata huduma. Kwa hivyo, nilikuwa nimetarajia sana hali hiyo iweze kutajwa katika hotuba ya Mhe. Raia. Sisi sote tunajua vile hali ilivyo. Sehemu zote tatu za uwakilishi Bungeni za Kaunti ya Tana River zimeathirika zaidi. Ninaisihi Serikali ishughulikie zaidi sehemu ya Chafa katika Tana Delta na kutangaza janga hili kama la kitaifa. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, ninaunga mkono maswala yote katika hotuba hii."
}