GET /api/v0.1/hansard/entries/797834/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 797834,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/797834/?format=api",
    "text_counter": 208,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "May 9, 2018 SENATE DEBATES 33 Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana Bw. Naibu Spika. Kwanza kabisa, nataka kuunga mkono Hotuba ya Rais ambayo alitoa na pia kwa kutambua kiongozi aliyepigania uongozi mwema hapa kwetu Kenya, marehemu Matiba. Hapa Kenya, tunafanya maajabu kwa sababu sisi hupongeza viongozi wakati wamefariki. Kuna viongozi wengi ambao wamefanya mambo mazuri hapa nchini kama Mheshimiwa Paul Muite, Sen. Orengo, Mheshimiwa Charles Rubia na wengine ambao wamechangia sana katika kuboresha demokrasia lakini tunampongeza mtu wakati amekufa. Ni vizuri tuwatambue hata wale ambao wako hai ili mambo ambayo mtu alifanya yajulikana vizuri na tunampongeza akiwa hai badala ya kuwekelea maua katika kaburi lake. Nataka pia kumshukuru Rais kwa sababu alitambua ugatuzi na vile ambavyo ugatuzi unaendelea. Ukiangalia vile pesa zilivyo kuwa zikitolewa, utaona kwamba Serikali ilikuwa inatoa Ksh210 bilioni kwa ajili ya serikali za kaunti lakini kiwango hicho kina zidi kuongezeka. Tunajua kwamba Serikali kuu imetoa Zaidi ya Ksh300 bilioni kwa serikali za kaunti. Kwa hivyo,mimi napongeza Rais wataifa. Jambo ambalo limekuwa changamoto kwetu kama maseneta ni ya kwamba kunasemekana kwamba ufisadi umekithiri sana katika kaunti zetu na hiyo ni kazi yetu kama maseneta. Tunafaa kuangalia kwamba pesa ambazo zimekwenda mashinani zinatumika kwa kazi ambayo zimetengewa kufanya pale mashinani; bali si kuwatajirisha watu wachache na kuwafanya wengine kuweza kujenga manyumba kama vile mheshimiwa Rais alivyosema. Unapata mtu ameajiriwa juzi, lakini baada ya miezi miwili au mitatu, amejenga nyumba ya orofa. Sisi kama Seneti tunazembea kidogo katika kazi yetu na tutajitolea kabisa ili tuweze kuangaliana kumulika vizuri pesa ambazo zinakwenda katika kaunti. Jambo linguine ambalo ningependa kusema ni ya kwamba alizitaja nguzo nne ambazo yeye mwenyewe anaziamini zitasaidia kuimarisha Maisha ya watu wetu. Jambo la kwanza, nikupigana na janga la njaa. Waziri ambaye anashughulika na mambo ya ukulima tayari ameanza kutengeneza mabawa katika sehemu nyingi."
}