GET /api/v0.1/hansard/entries/797839/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 797839,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/797839/?format=api",
    "text_counter": 213,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "alimsalimia mtu mmoja. Nimetoka katika jamii ya wafugaji na ninajua ya kwamba wakati ng'ombe ameumwa na simba, unamtafuta simba lakini husumbuki na wale nzi wanaobaki wakilambalamba damu. Kuna ndugu wangu wengine ambao hawataki tuongelee kuhusu mwaka wa 2022. Tunafaa kuongea ili tuweze kujiuliza mambo kama vile, tutaweza kujenga daraja na hospitali ngapi, tutakuwa na walimu wangapi na tutakuwa tumepeleka stima kwa nyumba ngapi, inapofika mwaka wa 2022. Baada ya kuongea hayo, tutajiuliza ni nani atakeyekuwa kwenye mstari wa mbele hayo mambo yakifanywa. Tukijiuliza hayo, tutakuwa na jawabu. Vile ambavyo Rais amesema, sisi wote tunafaa kuomba msamaha kwa wale ambao tumekosea na tutembee pamoja. Bw. Naibu Spika, Nitakomea hapo. Ahsante kwa kunipa fursa hii ili niweze kuongea kuhusu hotuba ya Rais."
}