GET /api/v0.1/hansard/entries/797860/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 797860,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/797860/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "May 9, 2018 SENATE DEBATES 38 Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia hotuba ya Mhe. Rais Kenyatta. Kwanza, ningependa kuipongeza hotuba kwa kukariri Uhuru wa mahakama. Itakumbukwa kuwa mwaka uliopita, baada ya sisi kupiga kura na Mahakama Kuu Nchini kutoa hukumu yake na kuagiza uchaguzi wa uraisi urudiwe, Mhe. Rais alionenekana akishtumu sana mahakama. Kwa hivyo, yeye kukariri uhuru wa mahakama mbele ya Bunge ilikuwa ni jambo kubwa sana ambalo lazima tumpongeze. Mahakama ndiyo inayoamua juu ya mizozo baina ya raia, vitengo tofauti vya uongozi na taasisi tofauti katika nchi. Kwa hivyo, uhuru wake ni muhimu katika kujenga demokrasia katika nchi yoyote ulimwenguni. Jambo la pili ambalo ningependa kuipongezea hotuba ya Rais ni swala la usalama. Ijapokuwa Mhe. Rais alijipigia debe kwamba ameweza kupunguza visa vya utovu wa usalama katika maeneo mengi, tunapata kwamba bado visa hivyo vinaendelea katika sehemu tofautitofauti. Nikizungumzia Kaunti ya Mombasa, kuna sehemu tofauti ambazo zina ukosefu wa usalama. Kwa hivyo, tungeomba Serikali itumie fursa hii, hasa tunapoelekea katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kuhakikisha kwamba usalama wa kutosha katika mji wa Mombasa na maeneo mengine ambayo Waisilamu wanaishi kwa wingi. Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kuna sala za usiku. Kwa hivyo, ni lazima wahakikishiwe usalama wao wanapokwenda au kutoka katika ibaada hizo. Kuhusiana na mambo ya usalama, tumeona kwamba mwaka jana baada ya kura, watu kadhaa walipoteza maisha yao mikononi mwa polisi. Polisi wanatarajiwa kuwa wakiwapatia raia usalama, lakini walikuwa mbele kuuwa raia, kuharibu mali na mambo mengineo ambayo hayafai.Tunasema kwamba wakati Serikali inapoagalia mambo ya usalama, inapaswa pia kuwafunza upya polisi wote ili wahakikishe kwamba wanalinda maisha na mali ya raia. Bw. Naibu Spika, swala la tatu ambalo ningependa kuliguzia ni lile la afya. Tunaunga mkono afya kwa wananchi wote wa Kenya. Hata hivyo, tunaona pia kwamba Serikali haijakuwa na uhakika kama kweli wanataka kusambaza afya kwa wote nchini Kenya. Tukiagalia, kwa mfano, katika mambo ya elimu,wameweza kutoa mipango ya kupeleka vipakatalishi katika kila shule ya msingi katika nchi ya Kenya. Hata hivyo, wameshindwa kupele vipakatalishi zile katika vituo vya afya katika nchi ya Kenya ili viunganishwe na Hospitali Kuu ya Kenyatta. Kwa mfano, kule Tiaty sasa kuna mkurupuko wa maradhi ambayo hayajulikani. Hii ingewezesha mgonjwa akienda katika kituo cha afya, kwa mfano huko Tiaty, ugonjwa wake unawezakuangaliwa na ripoti ikawasilishwa mpaka kwa Hospitali Kuu ya Kenyatta ambayo ndiyo hospitali kuu ya kuelekezwa wagonjwa nchini Kenya. Tunaona kwamba hakuna mipango yoyote ya kuweza kupeleka vifaa vya Kisasa kama vile kompyuta ili wagonjwa wanao hudhuria katika hizi taasisi za afya maelezo yao ya wezekuchukuliwa na yawazilishwe katika Hospitali Kuu ya Kenyatta. Jambo hili linaweza kuhakikisha kwamba magonjwa yaleyanaweza kuangaliwa kwa uangalifu zaidi ili kupunguza kupoteza maisha kupitia vifo ambavyo vinaweza kuepukika. Pia tumeona kwamba katika nchi ya Kenya hivi sasa kuna hatari ya kurejea kwa ugonjwa wa Polio. Polio imesababishwa na maji ambayo yameingiana na virusi vyake katika maeneo fulani nchini Kenya. Haya nilicha ya kuwa, mwaka uliopita Polio ilikuwa karibu kuondolewa kabisa katika nchi ya Kenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}