GET /api/v0.1/hansard/entries/797862/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 797862,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/797862/?format=api",
    "text_counter": 236,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Tungeiomba Serikali ituletee vifaa vya kimsingi badala ya kutuletea mashine kubwa za utafiti au za kupima Saratani ama maradhi mengine makubwa. Inafaa tuwe na vitu vidogo vidogo kama kuwa na tarakilishi na vifaa vya kisasa katika zahanati zetu. Vifaa hivi vinampa mgonjwa nafasi ya kuangaliwa kwa urahisi bila kutembea muda mrefu ama kufunga safari ili kupata huduma za kiafya za kisasa. Afya kwa wote ni jambo nzuri na ni lazima tuliunge mkono. Bw. Naibu Spika, jambo la nne ni kuhusu ukulima ambao ndiyo ngao ya nchi yetu. Hii ni kwa sababu ukulima ndiyo utatupa chakula cha kutosha katika nchi yetu ya Kenya. Vilevile, utatupa fursa ya kupata viwanda ambavyo vitatusaidia kuifanya Kenya kuwa nchi ambayo imetajirika kiviwanda. Hata hivyo, tunaona kuwa ukulima wetu mwingi unategemea mvua. Mvua kwa sasa iko kwa wingi lakini hakuna mipango yoyote ambayo serikali imewapa watu kuhakikisha kwamba yale maji ya mvua ambayo yanatiririka kwa wingi yanaweza kuhifadhiwa na kuwekwa katika mahali pazuri ili yawezekutumika muhula ujao. Kutokana na hasara hii miji mingi imeweza kuharibika. Kwa mfano, katika Kaunti ya Tana River tumeambiwa kuwa vijiji 30 vimezama. Tumeshuhudia haya katika vyombo vyetu vya habari.Vilevile kaunti ya Kilifi na sehemu za Ganze zimeathirika. Kuna sehemu zingine tofauti ambazo zinaathirika na mvua kwa sasa. Bw. Naibu Spika, tunaona kwamba mengi ya mabwawa yanayojengwa ni kwa minajili ya watu kujinufaisha kibinafsi kupitia kula rushwa. Hata hivyo, kwa hakika mabwawa yale hayajaweza kusaidia miradi ya kuhifadhi maji, kuhakikisha kwamba wananchi hawapati shida katika sehemu zile.Mfano, ni ule mradi wa Galana-Kulalu ulikuwa umetarajiwa kusaidia kupunguza mafuriko na pia maji hayo yatumike katika zile sehemu ambazo zinafaa kutumika kwa ukulima lakini kwa sasa haijawezekana. La tano ni kuhusiana na ufisadi. Ni kweli kwamba mwaka wa 2013 katika hotuba kama ambayo aliyoitoa juzi, Mhe. Rais alizungumzia maswala fulani ya ufisadi na akataja majina katika Bunge lakini kutoka mwaka wa 2012/2013 mpaka sasa hatujaona matokoe yoyote kuhusu ufisadi, kama vile, watu kuhukumiwa mahakamani au watu kuonyeshwa kwamba hii ilikuwa ni mali ya ufisadi, tumeweza kuirejesha kwa serikali kupitia labda kwa mahakama ama Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi. Bw. Naibu Spika, ufisadi ni hatari kubwa inayotukabili hivi sasa. Kura za kitaifa nyingi zinapigwa kwa mirengo ya ufisadi kwa sababu wakati wengi wakienda mashinani kuomba kura, wanatumia fedha kama kigezo cha kuchaguliwa. Kwa hivyo, ufisadi ni jambo ambalo ni hatari kubwa kwa uhuru wa kila aina katika nchi Kenya. Unaambiwa, “Mwenye pesa mpishe.” Kwa hivyo, tusipopigana na ufisadi, ipo hatari ya taifa letu kuingia katika misukosuko zaidi siku za usoni. Katika hotuba ya Rais sikuona jambo lolote ambalo alilizungumzia akitaja kupambana na ufisadi kama njia ambayo twaweza kuiokoa nchi yetu ya Kenya katika siku za usoni. Lazima tupigane na ufisadi kwa njia yoyote. Ufisaidi haupo kwa serikali kuu pekee yake. Uko pia katika serikali za kaunti ambazo tumesema zitaleta maendeleo katika nchi yetu ya Kenya. Bw. Naibu Spika, ningependa kuzungumza juu ya uwiano ama “ handshake” ambayo ilifanyika baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Mhe. Raila Amolo Odinga. Kwa hakika, uwiano ule ama handshake ile imeleta mabadiliko katika nchi yetu ya Kenya. Leo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}