GET /api/v0.1/hansard/entries/797867/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 797867,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/797867/?format=api",
"text_counter": 241,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Samahani Bw. Spika. Sen. (Dr.) Langat ambaye ni Seneta wa Bomet anaweza kuongea nami ana kwa ana bila tashwishi yoyote kwamba anaweza kuripotiwa sehemu fulani kwamba amevunja sheria au mwafaka walio nao. Seneta wa Laikipia pia amezungumza kwa ufasaha kuunga mkono uwiano na akatoa mfano wa kupigana na simba ambaye anakula nyama na ukawaacha inzi ambao wanarukaruka pale. Ni jambo nzuri ambalo limekuja katika nchi yetu ya Kenya. Tuliunge mkone ili makabila yote au jamii zote katika nchi ya Kenya waunganishwe katika serikali ambayo twataka kuitumikia ili kuhakikisha kwamba yale matatizo tuliyokuwa nayo ya kura yanakwisha. Ni wazi kwamba kutokana na mwafaka huo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka lazima iundwe upya na tupate watu ambao wana tajriba ya kuhakikisha kwamba wanaweza kusimamia taasisi hii bila matatizo. Kura nyingi zimeharibika kwa sababu ya kutokuwa na imani na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka. Lakini nataraji kwamba katika tume ambayo itaundwa upya, itahakikisha kwamba haya hayarudiwi tena. Mwisho ni kwamba tusiogope wazo la kura ya maoni. Sisi kama Wakenya tuko huru kujadili swala lolote ambalo twaweza kulijadili tupate mwafaka. Hakuna mtu ambaye anatushikia, kwa mfano, bunduki kusema kwamba lazima tusizungumzie kura ya maoni. Kura ya maoni ni haki yetu. Lazima tuketi chini kama Wakenya tuzungumze ni mambo gani ambayo tutapeleka kwenye kura ya maoni, ni mambo gani ambayo tunataka tupitishe katika sheria ambayo itahakikisha kwamba kura zinazofuata ama usimamizi wa nchi yetu kwa siku zijazo utakuwa ni wa amani, uhuru na upendo kwa kila Mwanakenya. Bw. Naibu Spika, kwa hayo mengi, nashukuru kwa kunipa fursa hii. Ninaunga mkono hotuba ya Rais."
}