GET /api/v0.1/hansard/entries/798593/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 798593,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/798593/?format=api",
"text_counter": 164,
"type": "speech",
"speaker_name": "May 15, 2018 SENATE DEBATES 28 Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kujiunga na Seneta wa Kaunti ya Nakuru, Sen. Kihika, na Maseneta wote kuomboleza vifo vya watu takribani 50 kutokana na mkasa wa kupasuka kwa bwawa la Solai. Jambo la kusikitisha ni kwamba mkasa kama huu umetokea wakati huu ambao nchi yetu inajivunia kupiga hatua kimaendeleo ya kila aina. Ni wazi kwamba mikasa kama hii itaendela kutokea kutokana na utepetevu ambao unafanyika kati ya wafanyikazi wa Serikali na mashirika yasiyokuwa ya serikali. Nachukua pia fursa hii kuwatia moyo watu wa Kaunti ya Nakuru na hususan Sen. Kihika kwamba haya mambo asiyaachie hapo. Tuliona kwamba mwaka wa 1993 kule Mombasa wakati Ferry ya Mtongwe ilipozama, watu 250 walipoteza maisha yao. Jambo la kusikitisha ni kwamba hadi wa leo wale wahanga wa mkasa huo hawajalipwa. Serikali imeweka ahadi mara kwa mara kwamba watalipwa lakini bado haijatimiza. Mikasa kama hii itaendelea kutokea hadi wakati tutakaa chini kama wananchi wa Kenya na kusema kwamba yametosha na wale wanaosababisha mikasa kama hii lazima wafungwe ili kuhakikisha jambo kama hili halitokei tena. Bw. Naibu Spika, miaka miwili iliyopita, wakati ferry ilizama nchini Korea Kusini Waziri Mkuu alijiuzulu."
}