GET /api/v0.1/hansard/entries/798626/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 798626,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/798626/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Nampongeza Sen. Kihika kwa sababu ya kuleta Hoja hii Bungeni, hususan kwa sababu yeye pia juzi, alikuwa na mkasa wa wale vijana ambao walipoteza maisha yao wakiwa katika shughuli zao za kampeni. Pia, ni mama mwenye nguvu kwa sababu kama Seneta wa Kaunti hiyo, basi ni wajibu wake kutetea watu wake. Mhe. Naibu Spika, jambo la kushangaza ni kwamba unaposikiza vile ambavyo watu wanasema kuhusu hayo mabwawa ya Bw. Patel, ni kana kwamba, hakukuwa na ubaya wowote uliotendeka, ilhali tuna ona kwamba kumekuwa na uharibifu wa mali kwa hali ya juu.Watu pia, wamepoteza maisha yao. Swala kubwa ambalo lina jitokeza ni kwamba, katika nchi hii, kuna sheria za mabwanyenye na za makabwela. Maisha ya watu duni hayashughulikiwi kwa sababu wao wanakufa kiholela holela. Kulingana na kanuni za kutengeneza mabwawa ya maji, ni kwamba lazima bwawa likae kwa miaka zaidi ya 50 ama100. Hata hivyo, ni lazima ujenzi wake uwe unaweza kustahimili miaka 1,000. Hilo hatujaona likitendeka. Tunasikia wakisema kwamba ni kwa sababu ya mvua, ilhali mvua ilitarajiwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}