GET /api/v0.1/hansard/entries/799227/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 799227,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/799227/?format=api",
    "text_counter": 132,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Asante sana Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono Hoja hii ya kusitisha vikao vyetu ili twende kuhudhuria kongamano ambalo ni muhimu sana. Hata hivyo, kuna mambo tata ambayo yanajitokeza kuhusu vile serikali gatuzi zinafanya kazi zao. Hivi leo Gavana wa Nairobi, Gov. Mike Sonko, amependekeza kumteuwa Bw. Miguna Miguna ambaye amesema: “I am not boarding.” Kwa hivyo, jambo hilo limetupiliwa mbali. Inaonekana tulikosea mahali. Kuna magavana ambao wamejitokeza tayari kama mashabiki wazuri wa maendeleo. Kwa mfano, kuna Gov. Oparanya ambaye tulipokuwa katika kongamano la ugatuzi, tuliona maendeleo ambayo amefanya. Vile vile, Gov. (Prof.) Kivutha Kibwana amewapa watu wake afya huru kulingana na zile Ajenda Nne kuu za Serikali. Gov. Chepkwony pia hajawachwa nyuma katika maendeleo. Swala kuu ambalo tutapeleleza ni kwamba hulka ya yule ambaye anachaguliwa kuwa gavana wa kaunti ni muhimu sana kwa maendeleo ya kaunti hiyo na nchi yetu ya Kenya. Bi. Spika wa Muda, nashukuru kwamba Sen. Sakaja amesema kwamba kiwango cha utendakazi cha MCAs ambao walichaguliwa kimeongezeka sana. Leo tulikuwa na kikao na wawakilishi wa bunge la Kaunti ya Bungoma na wametuonyesha dhahiri shairi kwamba wanaelewa mambo ambayo wanafaa kuyazungumzia katika kamati husika. Ningependa kuzungumzia mambo au ajenda ya watu wenye ulemavu. Naliwakilisha kundi hili pamoja na dada yangu, Sen. (Dr.) Musuruve. Serikali gatuzi bado hazijatilia maanani vipengele vya sheria na sera ambazo zipo katika kiwango cha kitaifa kuhakikisha kwamba pia wanawahudumia watu wenye ulemavu katika kaunti zao. Ndiposa tutakuwa na kikao na wabunge wa serikali gatuzi siku ya Jumapili ili tuweze kuendeleza nadharia zetu na malumbano ambayo tulikuwa nayo katika hoteli ya Safari Park wiki iliyopita. Ni muhimu sana kuwa na agenda fika ya watu wenye ulemavu. Hususan, lazima kuwe na sheria kuhusu watu wenye ulemavu katika kila kaunti. Nampongeza Mhe. Abuka ambaye anatuwakilisha katika Kaunti ya Nairobi na vile vile Mhe. Carol Agwanda na vile vile mwakilishi wetu katika Kaunti ya Homa Bay. Hata hivyo, tungependa kuona kila serikali gatuzi ikipeana nafasi kwa wabunge wao wa kaunti kupitisha sheria kuhusu watu wenye ulemavu na vile vile bajeti ambazo zitawezesha miradi ya maendeleo kutekelezwa na mawiziri husika katika kaunti. Ni idadi ipi ya watu walemavu ambao wameajiriwa na serikali hizi? Kipengele cha 54(2) cha Katiba kinasema asilimia tano ya watu wote ambao wako katika nyadhifa za uongozi ama uteuzi wawe ni watu wenye ulimavu. Jambo hili halijawahi kutendeka. Hii warsha ni muhimu sana. Kuna maswala ambayo tutauliza kama watu wa Kaunti ya Kiambu. Kwa mfano, kwa nini serikali hii imetengewa kiasi cha chini cha pesa ikilinganishwa na mwaka uliopita? Pia tutaangazia swala la mvutano kati ya Wabunge wa Kaunti (MCAs) na magavana wao. Warsha hii itatupa nafasi kama Maseneta ya kuelewa sheria ambazo tunaweza kupitisha ili kuthibiti mfumo wa ugatuzi. Ni jukumu la Seneti kutunga sheria ambazo zitawezesha serikali za ugatuzi kuyafikia malengo yao. Kama vile tunavyosukumana na wenzetu katika Bunge la Kitaifa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}