GET /api/v0.1/hansard/entries/799273/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 799273,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/799273/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kule Mombasa. Vile vile nilipata fursa hivi Karibuni kusafiri West Pokot, Trans-Nzoia, Bungoma na Busia tukiandamana na Kamati ya DelegatedLegislation . Ni kweli kwamba waakilishi wa bunge za kaunti wana matatizo mengi kwa sababu hata kule West Pokot, ijapokuwa Spika ni mwanamke, lakini wale wabunge wa bunge la kaunti wanasema, “asante Madam Speaker, Sir.” Kwa hivyo hizi ni changamoto na ni kweli kwamba wale wabunge wa bunge la kaunti – namwona ndugu yangu, Sen. Poghisio ambaye ni mwenyekiti na Seneta wa West Pokot anatabasamu kwa jambo hilo. Haya ni mambo ambayo lazima tutoe mwongozo kwa haya mabunge ya kaunti. Vile vile wale wabunge wa zile kaunti wanataka fursa ya kufanyiwa ile tunaita kwa Kiingereza “mentorship ” kwa sababu wengi ni mara yao ya kwanza kuchaguliwa na wana hamu ya kuchangia katika bunge la kaunti lakini wanapata matatizo kadha wa kadha ya kutoweza kujitanasua ili wawezi kutoa mchango wao kikamilifu. Bi Spika wa Muda, tumezungumzia kwa uchache kuhusiana na Mswada unaokuja wa Ward Development Fund . Hiyo haitakuwa tiba ya yale matatizo yote ambayo yako katika kaunti kwa sababu tunaona kwamba viongozi wana changamoto nyingi ambazo nyingine zinawashinda kujieleza kikamilifu katika mabunge ya kaunti. Hata iwapo sheria ile itapita, itakuwa ni vigumu wao kuweza kuhakikisha kwamba zile fedha ambazo zinatakikana kutengwa katika zile wodi wanazowakilisha zinaweza kufika kule na kuwasaidia kuleta miradi. Hii ni kwa sababu, kwa sasa unapata kwamba, kwa mfano, hapa Nairobi, ijapokuwa Sen. Omanga amezungumzia kwamba kulikuwa na matatizo yaliyotokana na"
}