GET /api/v0.1/hansard/entries/799852/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 799852,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/799852/?format=api",
    "text_counter": 211,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ya kuunga mkono Hoya ya Sen. (Dr.) Gertrude Musuruve. Kwanza kabisa, Kiswahili ni lugha ya taifa kulingana na Katiba. Ni haki ya watoto wetu wenye ulemavu wa maskio kufunzwa kwa lugha ya Kiswahili. Hiyo ni haki yao ya Kikatiba. Sisi kama Bunge la Seneti tunapaswa kuwahakikishia kwamba haki hiyo inatimizwa. Jambo la pili ni kwamba ukosefu wa mtaala wa Kiswahili kwa wale ambao wana ulemavu wa maskio ina maana kwamba tunawanyima haki yao ya kikatiba kufunzwa kwa lugha ambayo wanaitaka. Katika sehemu nyingi katika Jamhuri ya Kenya, watu wanazungumza Kiswahili kama lugha yao ya kwanza. Hii ina maana kwamba wale ambao wanakwenda shule wakiwa na ulemavu wa maskio wanakosa kupata fursa ya kufunzwa mtaala kwa lugha ya Kiswahili. Pia inamaanisha kwamba mbali na kuwa wanabaguliwa kama walemavu ama wasiojiweza, ina maana pia wanabaguliwa katika kufunzwa masomo shuleni. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}