GET /api/v0.1/hansard/entries/799854/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 799854,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/799854/?format=api",
    "text_counter": 213,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ni aibu kwamba kwa wakati kama huu ambapo lugha ya Kiswahili ni moja ya masomo ambayo yanatahiniwa katika darasa la nane na kidato cha nne hadi chuo kikuu, hatuna mtaala wa Kiswahili ambao unaweza kufunzwa wale ambao wana ulemavu wa maskio. Bw. Naibu Spika, haki ya elimu pia ni haki ya kikatiba. Kwa hivyo, tunapowanyima fursa hawa wanafunzi wenye ulemavu wa maskio kufunzwa masomo fulani kwa lugha ya Kiswahili, ina maana kwamba tunawanyima pia haki yao ya kupata elimu kwa lugha wanayoweza kuitaka. Kama alivyotangulia kusema Sen. (Dr.) Musuruve kwamba lugha ya Kiswahili ina nafasi ya kuiunganisha Kenya nzima, ikawa tunazungumza kwa lugha moja kama ndugu zetu Watanzania ambapo zaidi ya makabila 100 yanazungumza lugha ya Kiswahili kama lugha yao ya mama. Hapa nchini Kenya, lugha ya Kiswahili kinatumika labda kwa biashara ndogo ndogo lakini ni lugha ambayo ina uwezo wa kuiunganisha Kenya nzima ikawa tunazungumza kwa lugha moja. Hata hapa katika Seneti, ni aibu kwamba hii OrderPaper haijatafsiriwa kwa Kiswahili. Kuna watu hapa ambao wana uzoefu mkubwa wa lugha ya Kiswahili na wangependa kujadili na kuchangia Hoja kwa lugha ya Kiswahili. Bw. Naibu Spika, tungependa kuona kwamba Hoja hii ambayo imeletwa na Sen. (Dr.) Musuruve inatiliwa maanani na mtaala wa Kiswahili kwa wale ambao wana ulemavu wa maskio unachapishwa na wanafunzwa mpaka chuo kikuu iwapo watakuwa na uwezo wa kusoma hadi chuo kikuu. Jumamosi iliyopita, tarehe 26, nilibahatika kuwa na mikutano na walemavu katika eneo la Bombolulu, Mombasa. Kwa hakika hali yao ni ya kusikitisha. Inakuwa shida kupata vitambulisho vya walemavu kwa sababu hawawezi kulipa ada ya vitambulisho hivyo. Kuwapa fursa ya kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili pia kutawasaidia wanafunzi katika shule ambazo wanasomea. Tuwasaidie walemavu pia waweze kupata ajira na vile vile kuanzisha biashara ndogo ndogo ambazo zitawasaidia kuendesha maisha yao. Ni aibu kwamba maseneta wengi hapa hawana walemavu katika ofisi zao. Hiyo inamaanisha kwamba wakati walemavu wanapokwenda katika ofisi hizo kutafuta huduma na kukosa mtu kama wao, inakuwa shida kujiamini wanapohudumiwa kama raia wengine. Hoja hii imekuja wakati mwafaka kwa sababu mtaala mpya wa elimu utaanzishwa nchini. Hii ni nafasi mwafaka ya kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wa kusikia wanapata fursa ya kusomeshwa lugha ya Kiswahili kama wanafunzi wengine. Naunga mkono Hoja hii."
}